MAMA LULU JAMAN MMMH.....!!NI HATARI TUPU...SHUKA NAYO MWENYEWE HAPA..... | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Thursday, April 3, 2014

MAMA LULU JAMAN MMMH.....!!NI HATARI TUPU...SHUKA NAYO MWENYEWE HAPA.....

MAMA wa msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametupiwa 
tuhuma nzito kuwa ni mnywaji wa pombe sana hali inayomfanya mwanaye 
huyo alalamikie pembeni.

Chanzo kilicho karibu na familia hiyo kimeliambia Amani juzi kuwa, Lulu amekuwa 
akijituma kuhakikisha kila kitu kwenye familia kinakwenda sawa lakini mama 
yake amekuwa
 akimkwaza kwani kila wakati anamuomba fedha ambazo hutumia kwenda 
‘kupombekea’.

Chanzo kliliendelea kutiririka kuwa, kutokana na Lulu kuchoshwa na tabia 
ya mama yake kutaka fedha na kila jioni kwenda baa, aliamua kumnunulia 
bodaboda ambayo inamuingizia fedha ambazo inadaiwa pia, kila akizipata 
huenda baa kulewa.

“Mama Lulu analewa mpaka sana, halafu anamlalamikia mwanaye kwamba ni 
mgumu hali ambayo inamuweka Lulu njia panda,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo paparazi wetu alimtafuta Lulu, ikasemekana yupo 
safarini na hakuwa hewani. Mapaparazi wetu walimtafuta mama yake na kumsomea 
madai yanayoelekezwa kwake, cha ajabu aling’aka na kusema:

“Sijanunuliwa bodaboda na Lulu yeye ndiye kasema ameninunulia au? Kwanza 
simtegemei Lulu mbona alipokuwa gerezani nilikuwa ninaishi vizuri tu namlea 
mwanangu na 
mama yangu, iweje leo nishindwe
 
“Mimi sijawahi kunywa pombe, nimeokoka nampenda sana Yesu. Hao wanaosema 
nalewa ni waongo wamekosa tu la kusema,” alisema mama Lulu huku akizidi kuangua 
kicheko.
Mara kadhaa vyanzo tofauti vimekuwa vikipenyeza habari Global kwamba mama huyo amekuwa akionekana katika ‘viwanja’ tofauti vya kula raha, ikidaiwa kuwa ni mtumiaji 
mzuri wa ‘mambo yale’.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers