MAPYA KUHUSU MLIPUKO WA BOMU ARUSHA...WAHUSIKA KUNASWA KUILAINI..SOMA ZAIDI HAPA....! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, April 16, 2014

MAPYA KUHUSU MLIPUKO WA BOMU ARUSHA...WAHUSIKA KUNASWA KUILAINI..SOMA ZAIDI HAPA....!


 Baadhi ya majeruhi katika mlipuko wa bomu uliotokea Arusha 
wakiwa hospitali.
WATU waliohusika na kutega bomu linalohisiwa kuwa ni la kienyeji katika baa ya 
Arusha Night Park huenda wakanaswa kirahisi baada ya polisi kuchukua mitambo 
ya usalama (CCTV) iliyofungwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi. 
 Katika tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, jumla ya watu 17 walijeruhiwa, baadhi yao vibaya sana wakati wakinywa na kufuatilia katika televisheni michuano ya soka inayochezwa katika nchi mbalimbali barani Ulaya. 

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas aliyefika eneo la tukio haraka 
akiwa na kikosi cha ukaguzi wa mabomu, mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa 
Mulongo na wa wilaya ya Arusha, John Mongella walishuhudia majeruhi
 wakiondolewa na kupelekwa katika hospitali mbalimbali kwa ajili ya 
kupatiwa matibabu. 

Mmiliki wa baa hiyo, Joseph Karugendo alisema anaamini waliohusika na 
tukio hilo lililojeruhi wafanyakazi na wateja wao watapatikana kwani 
walifunga mitambo ya kufuatilia matukio ya CCTV. 

“Baada ya tukio lile polisi walifika, wakazingira eneo lile hivyo leo
asubuhi (juzi) polisi wameondoka na ‘monitor’ ya CCTV pamoja na 
mfanyakazi wetu mmoja kwa lengo la kwenda kufanyia uchunguzi wa 
picha hizo,” alisema mkurugenzi huyo. 

Mmoja wa wahudumu waliokuwepo wakati tukio hilo likitokea, Aneth Mushi, 
alisema alikuwa amebeba chakula cha wateja ndipo aliposikia kishindo 
kikubwa na kelele za watu zilizomfanya aangushe sahani za chakula na 
kukimbia. 

“Kwa kweli nasikitika sana watu wameumia na mimi ni Mungu tu 
kaniokoa vinginevyo ningeweza kuwa mmoja wa majeruhi,” alisema Aneth. 

Hili ni tukio la tatu la bomu kutokea kwenye Jiji la Arusha kwa kipindi 
cha mwaka mmoja ambapo jumla ya watu saba wamepoteza maisha huku 
wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa. 

Katika tukio la Mei 5, mwaka jana bomu lilirushwa kwenye Kanisa laKatoliki 
la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti ambapo jumlaya watu 
watatu walifariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Tukio la pili ni lile la Juni 15, mwaka jana ambapo bomu lilirushwa 
kwenye mkutano wa kufunga kampeni wa Chama Cha Demokrasia 
na Maendeleo, (CHADEMA) kwenye Viwanja vya Soweto ambapo 
jumla ya watu wanne walifariki dunia akiwemo mwanamke mmoja na watoto watatu.

Hata hivyo tayari mtu mmoja amefikishwa mahakamani kuhusiana na 
tukio la bomu kanisani.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers