NEWS: MBAKAJI ACHOMWA KISU NA MWANAMKE ALIYETAKA KUMBAKA HUKO SHINYANGA | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Tuesday, April 22, 2014

NEWS: MBAKAJI ACHOMWA KISU NA MWANAMKE ALIYETAKA KUMBAKA HUKO SHINYANGA

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla
Mtu mmoja  aliyejulikana kwa jina Stephen Philbert(30) mkazi wa Ngokolo mjini 
Shinyanga ameuawa kwa kuchomwa kisu wakati akifanya jaribio la kumbaka 
mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 katika eneo la Ngokolo mjini 
Shinyanga usiku wa mkesha wa pasaka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla amesema kuwa 
tukio hilo limetokea Aprili 20 ,mwaka huu saa tisa usiku.
Amesema  siku ya tukio mwanamme huyo alivunja dirisha la nyumba ya mwanamke 
huyo na kuingia ndani kisha kufanya jaribio la kumbaka lakini katika kujihami kwake 
ndipo mwanamke huyo alimchoma kisu kichwani ,akafariki dunia akiwa katika 
hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi.
credit:kandili yetu

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers