NJIA KUU ZA MAFANIKIO!!....SOMA HII ITAKUSAIDIA!! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Thursday, April 10, 2014

NJIA KUU ZA MAFANIKIO!!....SOMA HII ITAKUSAIDIA!!

1.JIAMINI
njia mojawapo ya kujiamini ni lazima ujikubali na usipende kujikosoa wala kufikiri mambo ambayo yatakufanya ukose amani.
kama hujiamini jaribu kusimama mbele ya kioo na ujiambie maneno ya kujisifia ambayo yatakupa nguvu na yatakayokufanya ujione wewe ni wa thamani sana hapa duniani.

2.THUBUTU
Watu wengi ni waoga wa kujaribu vitu,unakuta mtu anaanza kufikiri hasi(negative) juu ya jambo analotaka kufanya,hali hii inasababisha uwe na hofu ya kujaribu lile jambo na inakufanya ushindwe kujiamini katika maamuzi yako na .
siku zote unapotaka kufanya jambo jiambie kuwa nitaweza hata kama ni gumu kiasi gani na usihofie kushindwa au hasara yoyote inayoweza kujitokeza.

3.AINA YA WATU UNAOWASHIRIKISHA MAWAZO YAKO
Kuwa makini na watu unaowashirikisha mawazo yako,unapotaka kufanya jambo washirikishe watu ambao watakupa mawazo mazuri ya kujenga na si ya kukukatisha tamaa au kupotosha.
kuna baadhi ya watu hawapendi maendeleo ya wenzao,mtu kama huyu ukimshirikisha lazima atakupotosha au kukukatisha tamaa ili mradi tu basi aone umeshindwa.

4.MSHIRIKISHE MUNGU
Watu wengi hutegemea akili zao zaidi ndio maana unakuta wanapitia magumu katika kutafuta mafanikio au hawafanikiwi kabisa.
laiti binadamu tungetambua kuwa Mungu ndiye anayetoa na anaweza kuchukua vilivyo vyake mda wowote,basi tungemweka mbele katika mambo yetu yote tunayoyafanya ili tufanikiwe katika kila tunalohitaji.

5.MPANGILIO
Kila kitu ili kifanikiwe ni lazima kuwe na mpangilio maalum,hata nyumba inavyojengwa huanza kujenga msingi mpaka unafikia kupaua,inaenda 'step by step' haikuanza tu kuwa nyumba from no where.
kwahiyo ni vyema kupangilia hatua utakazopitia katika kufanikiwa kwako bila kuruka hata moja.
hii inahusiana pia na matumizi ya pesa,kupata pesa si kufanikiwa bali vitu ulivyovifanya vya maendeleo kwa kutumia hiyo pesa ndio mafanikio,hivyo basi hata matumizi ya pesa yana hatua zake,huwezi ukawa unashinda kwenye majumba ya starehe wakati hujui familia yako inakula nini,wanavaa nini n.k.

6.USIKATE TAMAA
Njia ya mafanikio si nyepesi wala haijanyooka,lazima iwe na milima na mabonde hivyo basi vikwazo unavyopitia visikukatishe tamaa bali vikufanye uwe imara kama mwamba.
na ujipe moyo kwamba siku moja utafika,hata matajiri wote duniani lazima kila mmoja ana historia yake juu ya magumu aliyoyapitia,so kaza buti utafika 'every successfully person have a pain story behind'.

7.JUHUDI
Ndugu yangu usitegemee kufanikiwa kama wewe ni mtu wa kukaa vijiweni kupiga stori au kusengenya watu,kuangalia leo flani ametokelezeaje?leo flani kafanya nini? na blaaa blaaa kibao.
lazima ufanye kazi kwa bidii.

yapo mengi sana yanayoweza kukfanaya ufanikiwe ila nikichambua yote sitomaliza leo fanya kwanza hayo machache kama unahitaji kufanikiwa katika maisha yako.

''IF YOU FAIL TO PREPARE,YOU ARE PREPARING TO FAIL"

Imeandaliwa na Jacqueline Lohaygoogle+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers