P FUNK AFUNGA NDOA YA SIRI | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Tuesday, April 22, 2014

P FUNK AFUNGA NDOA YA SIRI

Stori: Gladness Mallya
BAADA ya kuishi maisha ya kisela kwa muda mrefu, hatimaye mtayarishaji nguli wa muziki Bongo, Paul Mathyasse ‘P Funk’ ameoa kwa siri.
Mtayarishaji nguli wa muziki Bongo, Paul Mathyasse ‘P Funk’ wakati wa harusi yake.
Taarifa kutoka kwa chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo, lilichukua nafasi jijini Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita kwa usiri mkubwa.
Imeelezwa kuwa, P Funk aliamua kumuoa rasmi mzazi mwenzake, Samira baada ya kuishi naye kwa miaka kadhaa kama mke na mume lakini haikujulikana mara moja sababu za kuweka usiri katika tukio hilo la kheri.
Maharusi wakipongezwa na ndugu na jamaa zao baada ya ndoa.
“Jamaa (P Funk) amevuta jiko rasmi kwa siri kubwa lakini ameamua kufanya siri hata sijui ni kwa nini, tukio limechukua nafasi huku Arusha na watu kadhaa walialikwa lakini mastaa siyo wengi.
“Sherehe imefana, watu wamekula, wamekunywa kwelikweli maana misosi ilikuwepo ya kumwaga,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, katika harusi hiyo, kulikuwepo na ulinzi mkali wa watu kuzuiwa kupiga picha hivyo matukio mengi kushindwa kusambaa mtandaoni.
“Daah! Ilikuwa ngumu sana, watu hawakuruhusiwa kupiga picha, hata simu zilizotumika zilikuwa zaidi ni za bwana na bibi harusi na ndugu wa karibu,” kilisema chanzo.
Mke wa P Funky.
Paparazi wetu aliposhibishwa habari hizo na baadhi ya picha kuvuja katika Mtandao wa Instagram, alimvuti waya P Funk lakini simu yake ya kiganjani iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Pamoja na paparazi wetu kumtumia ujumbe mfupi na kujitambulisha, hadi tunakwenda mitamboni prodyuza huyo hakupokea huku geti la nyumbani kwake, Bamaga-Mwenge likiwa limefungwa pasipo kujulikana kama yumo au la!
credit:GPL

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers