PICHAZ...AJALI ALIYOPATA MSANII SHETTA...JIONEE MWENYEWE HAPA... | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Saturday, April 12, 2014

PICHAZ...AJALI ALIYOPATA MSANII SHETTA...JIONEE MWENYEWE HAPA...

Msanii Shetta wa bongofleva amepata ajali ya gari maeneo ya Minjingu 
akielekea Babati kwa ajili ya kufanya show ambayo maamuzi ya kuifanya 
yalikuja dakika za mwisho. Wakiwahi show kwa kutumia usafiri wa gari aina 
ya Noah, walipata hiyo ajali jioni ya April 11 2014 baada ya gari kupinduka 
wakati dereva akiwa kwenye jitihada za kumkwepa Punda. 

Kwenye gari hilo, Shetta alikua na Msaidizi wake pamoja na Waandaaji wa 
show ambapo hakuna aliepoteza maisha isipokua majeraha madogomadogo 
huku yeye mwenyewe akiumia kichwani na mguuni.

Screen Shot 2014-04-12 at 4.27.59 AM
Shetta alipelekwa hospitali lakini baadae aliruhusiwa kuondoka na kuendelea 
na safari japo haijajulikana kama aliweza kufanya hiyo show baada ya
 kugundua kwamba alikua ameumia kidogo.
Hii picha hapa juu ni ya Shetta kwenye eneo la ajali muda mfupi tu baada 
ya kutokea ambapo baadae aliandika >> ‘nashukuru Mungu nimetoka 
salama, kweli Mungu mkubwa maana nilijua leo ndio mwisho wangu,
 ajali ni mbayaa sanaaaa, thanks wote mlionipa pole tupo pamoja’

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers