PICHAZ..HATARI SANA..MAISHA YA 'VIDEO' YA OMMY DIMPOZ UINGEREZA NI SHIDAAA AISEEE...!JIONEE MWENYEWE HAPA...! | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Thursday, April 3, 2014

PICHAZ..HATARI SANA..MAISHA YA 'VIDEO' YA OMMY DIMPOZ UINGEREZA NI SHIDAAA AISEEE...!JIONEE MWENYEWE HAPA...!

Maisha ya Ommy Dimpoz kwenye script ya video yake mpya aliyoishoot hivi 

karibuni nchini Uingereza yanaonekana yalikuwa magumu sana.

Tayari staa huyo wa Tupogo ameshawaonesha mashabiki wake baadhi ya 
picha za uchukuaji wa video hiyo iliyoongozwa na Mnaijeria aishiye London, 
Uingereza, Moe Musa zikiwemo zile anazoonekana akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Muongozaji huyo wa video leo ameshare picha nyingine inayoonesha akiwa
 kwenye mchakato wa kuhariri video hiyo na tumegundua kitu kingine- Ommy 
alikufa kwenye video 
hiyo.. patamu hapo (kwa sauti ya Soudy Brown). 
Katika picha hiyo, Ommy Dimpoz anaonekana akiwa kwenye jeneza. “Color Grading/Correcting @ommydimpoz Music Video. Visuals look #Frosh2Death,” 
ameandika muongozaji huyo.

Hivi karibuni, Ommy Dimpoz alisema kabla hata ya kufahamu kuwa Sofia 
Skvortsova ndiye model atakayemtumia kwenye video yake, alikuwa a
memuona na akatamani msichana kama yeye aonekane kwenye video hiyo.

“Kwanza yule msichana wakati mimi natoka naelekea location, tupo kwenye taa hivi
 ambapo tunavuka taa ambazo ukizivuka unaelekea eneo la location nikawa namuona
 msichana yaani mzuri halafu nikawa nasema kimoyomoyo kwasababu nilikuwa 
sijamuona nikakutana naye location moja kwa moja, hatukukutana siku ya kwanza
 tukapanda, 
hapana, alikuja moja kwa moja siku ya kushoot,” Ommy aliiambia Bongo5.

Alisema baada ya kumuona Sofia alimwambia mshkaji wake kuwa anatamani 
msichana kama huyo awe kwenye video yake. Ameongeza kuwa siku ya 
kufanya video alipofika location akamkuta Sofia eneo hilo na kumchanganya zaidi Ommy.

“Baadaye Moe Musa ndio ananiita ananitambulisha ‘huyu ndio video model, sijui unamuonaje,” ameelezea Ommy. “Mimi nikamwambia, ‘mimi nimempenda sana’ mimi nilimuambia nataka msichana mzuri kulingana na uzuri wa nyimbo na maadhui ya nyimbo yalihitaji msichana mzuri.”
Ommy alida kuwa kama mambo yakienda sawa anafikiria kumleta Sofia Tanzania 
siku ya uzinduzi wa video hiyo. Tangu amtambulishe kwenye Instagram, Sofia 
amepata
 followers wengi kutoka Tanzania. “Alipata followers wengi kutoka huku kwahiyo 
akashangaa 
sana halafu akaappreciate.”

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers