Hii Ndiyo Jeuri Ya Pesa Ya Diamond Platnumz, Tazama Mamilioni Aliyotumia Kutengeneza Video Yake Mpya Huko Nchini Uingereza Ambayo Kaimba Na Iyanya Wa Nigeria | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Friday, May 30, 2014

Hii Ndiyo Jeuri Ya Pesa Ya Diamond Platnumz, Tazama Mamilioni Aliyotumia Kutengeneza Video Yake Mpya Huko Nchini Uingereza Ambayo Kaimba Na Iyanya Wa Nigeria

Baada ya Diamond Platnumz kuchomoa kiasi cha Dola 25,000 sawa na Tsh millioni 40 za kitanzania  kwa   director Clarence Peters wa Nigieria kwa ajili ya kufanya production ya video ya number one remix aliyomshirikisha Davido ambapo ilijumuisha gharama za kila kitu hadi models na dancers , sasa jamaa ameamua kuchomoa mpunga huohuo yaani Dola elfu 25 kwa director MoE Musa ambae anaishi na kufanya kazi zake nchini Uingereza  kwa ajili ya video yake mpya aliyomshirikisha Iyanya kutoka nchini Nigeria.
Gharama hizo za Dola elfu 25 ($25,000) hazitajumuisha gharama za kumsafirisha Iyanya kutoka Nigeria pamoja na malazi na kila kitu anapokua nchini Uingereza. Kwasasa Diamond Platnumz yupo nchini Ghana ambapo anategemea kufanya  kolabo nyingine na Davido itakayowahusisha pia Tiwa Savage wa Nigeria na Mafikizolo wa South Africa ikiwa ni kampeni ya kituo kimoja kikubwa cha TV barani Afrika
props : vibe

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers