WEMA, DIAMOND NA HALIMA KIMWANA WACHAFUA HALI YA HEWA | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Monday, May 19, 2014

WEMA, DIAMOND NA HALIMA KIMWANA WACHAFUA HALI YA HEWA

JAMBO limezua jambo. Pamoja na kuanza kwa kishindo safari yake ya kuelekea Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa ajili ya fainali za kuwania Tuzo za MTV Africa (MAMA), mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na baby wake, Wema Isaac Sepetu wamechafua hali ya hewa, Ijumaa Wikienda lilikuwa linarandaranda ndani ya nyumba.
Pamoja na kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye shoo ya kuwatambulisha wasanii wanaowania tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta, Dar, Diamond hakumpandisha Wema stejini kama kawaida yake, jambo lililozua kizaazaa.
Kuna muda mashabiki wake walipiga kelele wakimtaka Wema apande stejini lakini hakufanya hivyo.
Awali Diamond alipanda stejini mishale ya saa 8:00 akipishwa na msanii kutoka Sauz, Jigger ambaye alikuwepo kwa ajili ya kutoa sapoti kwa Mbongo Fleva huyo.
Msauz huyo alifanya shoo ya dakika 20 kisha akampisha Diamond ambaye aliingia na Kibao cha Uswazi Take Away Remix, ambacho ndani yake amemfagilia Halima Haroun ‘Kimwana’ ambaye ni hasimu wa mpenzi wake, Wema.
Baada ya kumaliza wimbo huo ndipo baadhi ya mashabiki wakasikika wakimwambia Diamond ampandishae Wema la sivyo watakinukisha.
Ishu hiyo iliendelea hadi jamaa aliposhuka stejini hapo.
Wakati Diamond akiendelea kufanya makamuzi yake hayo, Wema na Halima Kimwana wote walikuwepo ukumbini hapo na kwa bahati nzuri kama si mbaya walijikuta wote wakimshangilia Diamond, tena wakiwa VIP ya juu ambapo walikuwa wakiingia watu maalum.
Mwanahabari wetu aliwashuhudia wawili hao walipogeukiana kila mmoja alionekana kumwekea mwenzake uso wa mbuzi.
Hali hiyo ilidumu hadi Diamond alipomaliza shoo yake na Wema kushuka na kumuacha Halima Kimwana.
Baada ya shughuli za shoo Diamond alibaki na Halima Kimwana wakicheza disco. 
Kufuatia hali hiyo kwenye mitandao ya kijamii usiku huohuo, kuliibuka maneno mengi kutoka kila upande kuwa shoo ya Diamond ilichafuliwa na Wema na Halima Kimwana ambaye alidaiwa alijipanga kwenda kumfanyia fujo Wema kwa kuwa yupo upande wa Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Stori: Musa Mateja na Shakoor Jongo

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers