CATHY AFUNGUKA HAYA NA AJUTIA KUJIUNGA BONGO MOVIE!

Stori: Gladness Mallya
MSANII mkongwe kwenye filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kuwa anajutia maisha aliyokuwa akiishi kipindi alipokuwa Bongo Movie Unity kwani alipoteza muelekeo kutokana na ile kasumba ya kukaa Viwanja vya Leaders kila kukicha kwa mambo yasiyokuwa na tija.
Msanii mkongwe kwenye filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Cathy alisema kati ya vitu vinavyomuumiza ni kupoteza fedha nyingi kwenye vikao Leaders bila kuingiza fedha yoyote na sasa anajuta.
“Unajua sisi Wapare tumekuja mjini kutafuta hela sasa mimi nilikuwa natoa tu bila faida yoyote. Nilikuwa natumia pesa kununua mafuta ya gari kuendea pale, kununulia vinywaji na matumizi mengine lakini manufaa sijayaona.
“Namshukuru Mungu kwa sababu amenitoa kwenye hilo kundi na sasa nafanya kazi zangu za maana zaidi na ile tabia ya kukaa na kunywa au kutumia fedha kijinga haipo tena,” alisema Cathy.
CATHY AFUNGUKA HAYA NA AJUTIA KUJIUNGA BONGO MOVIE! CATHY AFUNGUKA HAYA NA  AJUTIA KUJIUNGA BONGO MOVIE! Reviewed by Linnah Lsquare on 9:58 PM Rating: 5
Powered by Blogger.