HATIMAYE DIAMOND PLATINUMZ AFUNGUKA KUHUSU BIFU NA DAVIDO!

Kwa mara ya kwanza Diamond Platnumz amezungumzia kile kinachoaminika kuwa ni beef kati yake na msanii wa Nigeria, Davido iliyotokana na ushindi wa Idris kwenye Big Brother Africa. 

Akiongea na waandishi wa habari jana baada ya kuwasili jijini Kampala, Uganda kwaajili ya kutumbuiza kwenye party ya mpenzi wake mpya, Zari The Bosslady, Diamond alisema watu walichukulia tofauti kauli yake.  

“Professionally hakuna kitu kama hicho, hatuna beef yoyote,” alisema. “Ni kwamba tu nadhani watu walichukulia visivyo. Hiyo ilikuwa ni lugha ya kisanii na watu waliitafsiri tofauti lakini hakuna kitu kama hicho,” aliongeza. 

Diamond anazungumzia kauli yake aliyosema usiku wa fainali za Big Brother baada ya yeye pia kutwaa tuzo ya TFA ya huko Nigeria. 

“Thanks God, we have Cheated another one on The Future Awards Africa in Lagos Nigeria… #SameDay #SameNight Thank you Allah,” aliandika kujibu tweet ya Davido ilisomeka: And They cheat Again.. Lol.” 

Katika hatua nyingine, akiongea na Ugandan Allstar, Diamond Platnumz alidai kuwa baba yake Mzee Abdul ana asili ya Uganda. “Ni kama nipo nyumbani sasa hivi,”alisema. 
“Sikujua kuhusu hilo, baba yangu anatokea hapa (Uganda).”
HATIMAYE DIAMOND PLATINUMZ AFUNGUKA KUHUSU BIFU NA DAVIDO! HATIMAYE DIAMOND PLATINUMZ AFUNGUKA KUHUSU BIFU NA DAVIDO! Reviewed by Linnah Lsquare on 3:31 AM Rating: 5
Powered by Blogger.