HIVI NDIVYO MADAHA ALIVYOFUNGUKA KUHUSU SKENDO YA KUJIUZA, KUTOKUWA NA PA’ KUISHI

Baby Joseph Madaha ndiye ambaye wiki hii yuko hapa kujibu maswali 10 ambayo mwandishi wetu Gladness Mallya alimuuliza. Ilikuwa hivi;
Staa Baby Joseph Madaha.
Ijumaa: Umekuwa ukitajwa kuwa wewe ni msanii wa kike unayeongoza kwa kubadilisha mabwana kila kukicha, hili likoje?
Baby Madaha: Ukweli hiyo huwa inatokea tu na huwa sipendi kusumbuliwa na mwanaume, nikiona ananizingua nammwaga. Hata hivyo, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza, nafanya kazi, mapenzi pembeni.
Ijumaa: Unadhani kwa nini umekuwa ukiingia kwenye uhusiano kisha kutoswa, ni umachepele wako au kitu gani?
Baby Madaha: Mimi wala siyo machepele kama watu wanavyonifikiria na kiukweli huwa nawaacha mimi na siyo wao kuniacha.
Ijumaa: Mpaka sasa umeshakuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wangapi?
Baby Madaha: Wanaume niliotembea nao ni siri yangu kwa sababu nikitaja idadi hapa watu watalia na wewe mwandishi unaweza kuzimia.
Ijumaa: Kuna tetesi kwamba wewe na msanii mwenzako Isabela Mpanda huwa mnaishi kama mke na mume, hebu eleza ukweli wa hili jambo.
Baby Madaha: Siyo kweli na sijawahi kufanya usagaji katika maisha yangu. Isabela ni rafiki yangu tunafanya kazi, hayo mengine ni maneno ya watu tu.
Ijumaa: Vipi kuhusu penzi lako na meneja wako, Joe Kariuki limeishia wapi? Mbona safari za Nairobi sasa zimepungua tofauti na zamani?
Baby Madaha: Mapenzi na Joe yameisha, kuhusu kwenda Nairobi nimepunguza kwa sababu nafanya kazi zangu za filamu. Mkataba wangu na kampuni ya Candy & Candy unaisha mwaka ujao na unaniruhusu kufanya kazi zangu za filamu, wao nafanya nao muziki tu.
Baby Madaha akila ujana.
Ijumaa: Kwa skendo hizo unadhani utapata kweli mwanaume wa kukuoa hadi ukawa na familia?
Baby Madaha: Achilia mbali hilo suala la skendo, mimi sina mpango wa kuwa na familia kabisa.
Ijumaa: Kuna habari kwamba huna sehemu maalum ya kuishi bali unaishi kwa marafiki tu, unalizungumziaje hili?
Baby Madaha: Huo ni uongo, mimi niko kwangu maeneo ya Kijitonyama na Jaffarai ni jirani yangu, hao wanaoongea hawana hoja.
Ijumaa: Wasanii wengi wa kike mnatajwa kwamba huwa mnafanya biashara ya kujiuza usiku ndiyo maana mchana mnalala mpaka jioni, vipi hapo?
Baby Madaha: Mimi sina hiyo tabia ya kujiuza ila huwa napenda sana starehe hivyo usiku mara nyingi natoka narudi nyumbani asubuhi.
Ijumaa: Unapata wapi hizo fedha za kufanya starehe kila siku wakati sanaa hailipi kihivyo?
Baby Madaha: Huwa naweka akiba, wanaosema sanaa hailipi naona hawajui kupangilia kile wanachokipata.
Ijumaa: Kwa sasa uko kimya sana na huvumi kama zamani, tatizo ni nini?
Baby Madaha: Unajua watu wanashindwa kuelewa mimi nina kazi tatu, uanamitindo, filamu na muziki hivyo nikiwa kimya kwenye kazi moja tambueni kwamba niko kwenye upande wa kazi nyingine maana mjini huwezi kutegemea kazi moja.
HIVI NDIVYO MADAHA ALIVYOFUNGUKA KUHUSU SKENDO YA KUJIUZA, KUTOKUWA NA PA’ KUISHI HIVI NDIVYO MADAHA ALIVYOFUNGUKA KUHUSU SKENDO YA KUJIUZA, KUTOKUWA NA PA’ KUISHI Reviewed by Linnah Lsquare on 9:50 PM Rating: 5
Powered by Blogger.