MADAI MAZITO: FLORA MBASHA AMFUNGULIA KESI YA TALAKA MUMEWE!

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Flora Mayala maarufu kama Flora Mbasha amefungua kesi ya madai  dhidi ya mume wake Emmanuel Mbasha kuomba talaka na kugawana mali walizochuma wakati wakiwa katika ndoa. 

Flora alifungua kesi hiyo namba 64/2014 katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam mbele ya hakimu Devotha Kisoka. 
Pamoja na maombi hayo Flora aliomba aruhusiwe kuishi na mwanae Elizabeth Mbasha mwenye miaka 11 na kwamba Mbasha ahusike katika kumuhudumia mtoto huyo.


Flora alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu ameumizwa,amekua na msongo wa mawazo na kwamba anahitaji mtu atakayekua mwangalifu naye na kumsaidia. 

Alieleza kwamba Mbasha alikua akimfanyia vitendo vya ukatili kwa kumshambulia kwa kipigo na baadaye kushindwa kutoa huduma na matibabu anapoumia na pia aliwahi kumtishia kumuua baada ya kuripoti ustawi wa jamii kuhusu mgogoro huo. 
MADAI MAZITO: FLORA MBASHA AMFUNGULIA KESI YA TALAKA MUMEWE! MADAI MAZITO: FLORA MBASHA AMFUNGULIA KESI YA TALAKA MUMEWE! Reviewed by Linnah Lsquare on 6:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.