Diamond Atoa Sababu za Kushindwa Kuhudhuria Msiba wa Baba yake Dully Sykes

Diamond Platnumz ni miongoni mwa marafiki wa karibu wa msanii Dully Sykes ambaye weekend iliyopita alimpoteza baba yake mzazi Ebby Sykes, lakini hakuweza kuhudhuria msiba huo kutokana na sababu ambazo amezitoa leo.

Diamond ambaye wakati msiba huo unatokea alikuwa Zanzibar na mpenzi wake Zari, ameelezea sababu zilizomfanya kushindwa kuhudhuria mazishi.

“Watu waliniona niko zanzibar lakini walikuwa hawajui nimeenda kufanya nini,” Diamond

ameiambia 255 ya XXL ya Clouds FM. “Usiangalie kila unachokiona Instagram ukajua mtu labda kwasababu alikuwa anafanya starehe.

Niko katika kipindi ambacho sio kizuri kwangu mimi na familia yangu kwasababu kuna vitu ambavyo siwezi kuvizungumza lakini, na siwezi kuviweka kwenye media ndo maana watu wengine wanaweza kuniona nacheka lakini […kwanza mama yangu anaumwa na anaumwa sana sijawahi kulizungumza hili ndo nalizungumza hapa, hapa ninapoongea na wewe yupo India, kuna vitu vingi vinaendelea, siwezi kusema nilikuwa Zanzibar nafanya nini
Diamond Atoa Sababu za Kushindwa Kuhudhuria Msiba wa Baba yake Dully Sykes Diamond Atoa Sababu za Kushindwa Kuhudhuria Msiba wa Baba yake Dully Sykes Reviewed by Linnah Lsquare on 11:20 PM Rating: 5
Powered by Blogger.