Haya Mengine Saba ya Yamoto Band Kwenye BBC Dira ya Dunia

Tuliziona pichaz Yamoto Band pamoja na story za wao kwenda zao London, Uingereza kupiga show, siku ya leo FEB21 muda mfupi baadaye watakuwa na show, watu wetu hawa saa chache zilizopita walikuwa kwenye Interview na mtangazaji Charles Hillary kwenye BBC Dira ya Dunia.

Swali la kwanza kuulizwa ilikuwa wapi lilikozaliwa jina la Yamoto Band? ;”Ukiachana na vitu vya motomoto ambavyo tunavitoa ni jina ambalo lilibeba nyimbo yetu ya kwanza.. Yamoto Band ni zao la Mkubwa na Wanae, kituo ambacho kinalea watoto wenye vipaji..“– Aslay.


Kuhusu ishu ya mtu anayewaandikia nyimbo zao; “Mara nyingi sana tunaandika wenyewe lakini tunashare idea na bosi wetu Mkubwa Fella.. Tunakaa naye na tunashare idea“– Aslay.

Hapa wanaongelea utofauti wa Yamoto Band na band nyingine; “Vitu vingi vishafanyika, uongozi wetu unataka sisi tuwe wapya ndio maana bendi unaona iko tofauti kwanza tuna umri mdogo.. nyimbo zetu zina dakika tatu nne tofauti na bendi nyingine..“– Maromboso.

Band nyingi zinavunjika, unadhani hii itatokea kwa Yamoto?; “Sisi tumekaa ni zaidi ya miaka minne tuko pamoja kabla ya Yamoto Band kujulikana tunajua nini maisha halafu tumetoka katika maisha magumu.. Sio rahisi leo unishawishi kwa vitu vidogo milioni mbili milioni tatu wakati tunategemea mamilioni mengi baadaye“– Aslay.

Ni nini siri ya umoja wao?; “Tumekaa muda mrefu sana kwenye tundu moja kwa hiyo tumeshazoeana hata tabia zetu.. Tumeshakuwa kama ni ndugu sasa na sio marafiki tena“– Bella.
Hapa Charles aliomba kuambiwa maana ya ‘Kupwelepweta‘; “Kupwelepweta ni kitu ambacho hakikutoshi, kama mimi nivae koti lako lazima linipwelepete…“– Aslay.

Hii ni sauti ya Interview yao yote nimerekodi BBC Dira ya Dunia, play kuisikiliza.
Haya Mengine Saba ya Yamoto Band Kwenye BBC Dira ya Dunia Haya Mengine Saba ya Yamoto Band Kwenye BBC Dira ya Dunia Reviewed by Linnah Lsquare on 11:19 PM Rating: 5
Powered by Blogger.