Mungu ni Mkubwa: Mama yake Diamond Arejeshwa toka India......Afya yake kwa sasa inatia Moyo | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Monday, February 16, 2015

Mungu ni Mkubwa: Mama yake Diamond Arejeshwa toka India......Afya yake kwa sasa inatia Moyo

Mungu ni  mkubwa :Mama mzazi wa Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’, amerejeshwa Bongo kutoka India ambapo afya yake imetengemaa.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya familia ya jamaa huyo, kimesema kwamba tayari 
 Sandra amesharejea katika hali yake ya kawaida na ndiyo maana akarudi Bongo baada ya kulazwa hospitalini nchini India kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa kupooza.

Mwanafamilia huyo alisema kwamba, Diamond na mama yake walirejea nchini wikiendi iliyopita baada ya kufanyiwa matibabu ya kina na madaktari kujiridhisha kwa hali ya juu dhidi ya afya yake ambapo waligundua hali aliyonayo kwa sasa imetengemaa hivyo wakamruhusu kurejea kuungana na familia yake.

Habari zilieleza kuwa kwa sasa bimkubwa huyo yupo fiti na anaendelea na mazoezi ya kawaida huku akimalizia dawa alizopewa na wataalam hao wa afya.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers