Rais wa Chuo cha CBE Ndani ya Ufisadi Mkubwa , Abambwa na Mamilion ya Pesa Chumbani Kwake | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, February 18, 2015

Rais wa Chuo cha CBE Ndani ya Ufisadi Mkubwa , Abambwa na Mamilion ya Pesa Chumbani Kwake

KIMENUKA! Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Ramadhan Kirungi amejikuta akiwa korokoroni ya Kituo cha Polisi cha Daraja la Salenda jijini Dar baada ya kudaiwa ‘kufoji’ saini ya benki ya wanachuo na kuchota shilingi milioni 31.Kwa mujibu wa chanzo makini, wizi huo unadaiwa kubainika baada ya makamu wake, Godfrey Modest kutumwa benki kwa ajili ya kutoa fedha ambazo cheki yake ilishasainiwa.“Yule makamu aliporudi chuoni alimweleza mhusika, akashagaa sana na hakuamini kilichotokea ndipo walipoamua kumkamata rais huyo.

“Walipokwenda kumkagua kwake walimkuta na shilingi milioni 16.5 keshi zilizosalia zikiwa zimefungwa katika mafungu matatu,” kilisema chanzo chetu kikiomba hifadhi ya jina lake.

Baada ya habari hizo kutua kwenye Gazeti la Amani, mapaparazi wetu walimtafuta msemaji wa chuo hicho, Leonidas Tibanga ambaye alikiri kutokea kwa wizi huo na kuongeza kuwa hatua zimechukuliwa na mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa polisi huku uchunguzi zaidi ukifanyika.“Ni kweli wizo huo umetokea na hivi ninavyozungumza na wewe, mtuhumiwa yupo polisi lakini uchunguzi zaidi unaendelea,” alisema Tibanga.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers