Unyama wa Kutisha, Mwanafunzi wa Chuo Abakwa na Kisha Kuuwawa Kinyama

Mwanafunzi mmoja wa kike kutoka Chuo cha Moi huko Eldoret, Kenya amekutwa amefariki dunia karibu na moja ya hosteli za chuo hicho baada ya kubakwa na kuuwawa kikatili.
Mwanafunzi huyo inasemekana kuwa ni wa mwaka wa tatu chuoni hapo akichukulia masomo ya Sanaa na Sayansi ya Jamii.

Tukio hilo la kinyama, limetokea usiku wa kuamkia leo na bado polisi haijawatia hatiani washtakiwa ama wahusika wa tukio hilo. Habari za mkasa huo zinazidi kuenea kila kona ya chuo, huku taharuki na hofu kubwa ikizidi kuwapanda wanafunzi wengine wa kike ambao wameamua kupaza sauti kuuomba uongozi wa chuo hicho kuimarisha suala zima la ulinzi kwa usalama zaidi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafunzi wa zamani katika chuo hicho, wamethibitisha kuwa tangu mwaka 2006, kumekuwa na matukio ya aina hiyo ambapo wanafunzi wengi wamekuwa wakikabwa na wengine kubakwa na watu wasiofahamika mara moja, hivyo wanafunzi kuwabatiza jina la ‘mashoka’,kutokana na wakabaji kutumia silaha za shoka katika kutekeleza azma yao.

Hata hivyo vitendo hivyo vilikoma kwa kipindi fulani, kuanzia mwaka 2011, hivyo tukio la jana linaashiria bado kuna kiza kinene kwa maisha ya wanafunzi chuoni hapo.
Unyama wa Kutisha, Mwanafunzi wa Chuo Abakwa na Kisha Kuuwawa Kinyama Unyama wa Kutisha, Mwanafunzi wa Chuo Abakwa na Kisha Kuuwawa Kinyama Reviewed by Linnah Lsquare on 10:35 PM Rating: 5
Powered by Blogger.