Wema Amuumbua Kajala!

UBUYU: Gazeti la udaku la Amani, limeripoti kuwa mrembo na mwigizaji wa Bongo Movies ,Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amedaiwa kumuumbua shosti wake wa zamani, Kajala Masanja kwa kumwaga ‘ubuyu’ kwamba amefilisika baada ya kigogo maarufu kama CK anayedaiwa kuwa ndiye mpenzi wake, kuyumba kiuchumi.

Kigogo huyo aliyewahi kuwa na uhusiano na Wema kisha kumwagana naye, imedaiwa kuwa ile jeuri ya kununua magari ya kifahari, kumiliki biashara mbalimbali mjini, kwa sasa ameangukia pua kwani hawezi tena kujitutumua.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na Wema, baada ya kuhamishia majeshi kwa Kajala, Wema hakufurahia hivyo aliposikia uchumi umeyumba, amefurahia sana kufuatia ule msemo wa ‘adui muombee njaa.’

“Wema amefurahi sana, anawaambia marafiki zake kuwa malipo ni hapahapa duniani, Wema alimlipia Kajala dhamana ya sh mil. 13 ili asifungwe kwa msala wa kutakatisha fedha uliokuwa ukimkabili lakini akamgeuka na kumchukulia bwana wake, ule si ubinadamu kabisa,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, Kajala ana nuksi kwani CK alipokuwa na Wema alikuwa na mafanikio na kupata fedha kila kukicha lakini alipohamia kwa Kajala mambo ndiyo yakaharibika.
“Kajala ana nuksi, CK alipokuwa na Wema walikuwa wanapata fedha nyingi kila wakati lakini kwa Kajala wamefilisika kwelikweli,” kilisema chanzo na kuongeza:

“Madam mwenyewe amemshangaa sana CK kuishiwa fedha wakati alikuwa mtu wa kucheza na dola nyingi kila kukicha na aliwekeza fedha zake katika miradi mbalimbali.”

Jitihada za kumpata CK ili azungumzie ishu ya kuyumba kiuchumi hazikuzaa matunda lakini kwa mujibu wa mmoja wa watu ambao wanafanya naye kazi, kigogo huyo ameporomoka kiuchumi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kufanya magumashi ya fedha kazini hadi kufikia hatua ya kutaka kufukuzwa kazi.

“CK hayuko vizuri kazini, ana majanga kibao, ile jeuri aliyokuwa akifanya na Wema na Kajala ilikuwa ni fedha za magumashi sasa kimemnukia kazini,” kilisema chanzo hicho ingawa mwenyewe alipotafutwa kwenye simu hakupatikana.
Wakati mwanahabari wa Amani akiendelea kuichimba habari hiyo, alifanikiwa kunasa ‘clip’ ya sauti ya Wema iliyoonesha dhahiri kwamba mrembo huyo amefurahishwa na kitendo cha wawili hao kukalia kuti kavu.

Sauti hiyo ya Wema inasikika akizungumza na shosti yake kumueleza jinsi gani Kajala ameumbuka maana alifikiri kutembea na shemeji yake ameula kumbe matokeo yake ameangukia pua kwani mwanaume amefilisika.“…Kajala sasa hivi anaendesha Noah (Toyota) ile yenye mastikamastika nakwambia…” ilisikika sehemu ya clip hiyo.

Paparazi wa Amaani alimvutia waya Wema ili aweze kufunguka zaidi kuhusiana na sakata hilo namna ambavyo amefurahia, simu yake iliita bila kupokelewa.Hata hivyo, mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwake, mtaa wa Bwawani-Kijitonyama jijini Dar zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti lakini hakufanikiwa kumpata baada ya mlinzi kudai amelala.

Mwanahabari wa Amani alimvutia waya Kajala ili kusikia naye anasemaje baada ya kudaiwa kuanguka kiuchumi, simu yake iliita bila kupokelewa lakini hata hivyo, rafiki yake wa karibu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alikanusha madai ya kufilisika.“Kajala hajafilisika na hawezi kufilisika, hayo yatakuwa maneno ya watu tu,” alisema rafiki huyo wa Kajala.

Wema na Kajala waliwahi kuwa mashosti wa damu kabla ya kugombana ambapo chanzo kilitajwa kuwa ni CK,  mwaka jana walidaiwa kupatana lakini baadaye ikaelezwa kuwa bado wanaendeleza bifu.
Wema Amuumbua Kajala! Wema Amuumbua Kajala! Reviewed by Linnah Lsquare on 9:19 PM Rating: 5
Powered by Blogger.