Haya Ndio Aliyoyasema Diamond Kuhusu Hali ya Wema Kutoshika Mimba

Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameeleza kulifahamu  kwa muda mrefu  tatizo la aliyekuwa mpenzi wake , Wema Sepetu la kutoshika mimba.
Akiongea na kipindi cha Ng’ari Ng’ari cha Clouds TV, Diamond alisema wakati wako pamoja waliwahi kuzunguka kwa wataalam mbalimbali kujaribu kupata tiba lakini hawakufanikiwa.
Alisema ilifika wakati alimweleza tu kuwa akubali hali hiyo.
Diamond alizungumzia pia lile andiko la Wema Sepetu mtandaoni ambapo alielezea tatizo
Akizungumzia andiko la Wema mtandaoni juu ya tatizo lake la kutoweza kupata mtoto, Diamond alisema aliumizwa na andiko hilo kama wengine walivyoumia, na alimsifu kwa kuusema ukweli japo hakufyrahishwa na watu walivyomshambulia kwa komenti za maudhi kwani anaumia kama  binadamu wengine.
Haya Ndio Aliyoyasema Diamond Kuhusu Hali ya Wema Kutoshika Mimba Haya Ndio Aliyoyasema Diamond Kuhusu Hali ya Wema Kutoshika Mimba Reviewed by Linnah Lsquare on 4:46 AM Rating: 5
Powered by Blogger.