NABII: WEMA ASIPOPATA MIMBA NDANI YA SIKU 21 NAACHA UTUMISHI

Musa Mateja
NABII wa Kanisa la The Revelation Church lililopo Buza-Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera amesema anao uwezo wa kumponya kwa maombi msanii wa Bongo Muvi anayesumbuliwa na tatizo la kutopata mimba, Wema Sepetu.
Msanii wa Bongo Muvi Wema Sepetu.
Akizungumza na mwandishi wetu kupitia msemaji wake, Nabii Yaspi alisema mwanamke yeyote aliyevunja ungo, amepewa na Mungu uwezo wa kuzaa isipokuwa shetani huingilia kati na kumnyima furaha mwanamke husika.

Nabii wa Kanisa la The Revelation Church Yaspi Bendera.
Nabii huyo alifunguka zaidi kwa kusema amemuuliza Mungu kupitia maombi kuhusu tatizo la Wema na kuona ana uwezo wa kulitatua, akimtaka msanii huyo kutojali imani yake ya dini, badala yake afike kanisani hapo ili amshike mkono tumboni mwake na kumuangushia maombi, kitu alichodai kitajibu ndani ya siku 21.
“Endapo ndani ya muda huo atashindwa kupata ujauzito, nipo tayari kuacha utumishi na kurejea zangu kijijini kuendelea na maisha mengine, maana kazi hii ni ya kiroho ambayo tunapewa maono na Mwenyezi Mungu,” alisema Nabii huyo.
NABII: WEMA ASIPOPATA MIMBA NDANI YA SIKU 21 NAACHA UTUMISHI NABII: WEMA ASIPOPATA MIMBA NDANI YA SIKU 21 NAACHA UTUMISHI Reviewed by Linnah Lsquare on 10:53 PM Rating: 5
Powered by Blogger.