Wema Amewatolea Uvivu ‘Miungu Watu’ Wanaomtoa Kasoro!

Staa wa mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu amewatolea uvivu baadhi ya watu ambao wameibuka kwa wingi mtandaoni wakiitoa karoso miguu ya staa huyo mara baada ya Wema kuweka picha kadhaa akiwa amevaa sketi amabayo inaonyesha miguu yake.
“Naomba niwaulize nyinyi mnaojiona miungu watu.... Mlitaka nijiongeze nyama miguuni kwangu au...? Ndo ilivyo na kuacha kuvaa nguo za kuionesha siwezi... Ntavaa tu... Yaani wala siwezi acha... Iwe mibaya iwe ina makovu iwe na michirizi ni ya Wema Sepetu... na kwakuwa ni yangu basi nita i embrace.. Tuko pamoja eeh... Sasa muache vifimbo vyangu... maana ndo Mungu alonibarikia navyo…” Wema ameandika kupitia ukurasa wake mtandaoni.
Picha: Wema Sepetu akiwa na dada yake Nuru Sepetu
Wema Amewatolea Uvivu ‘Miungu Watu’ Wanaomtoa Kasoro! Wema Amewatolea Uvivu ‘Miungu Watu’ Wanaomtoa Kasoro! Reviewed by Linnah Lsquare on 3:36 AM Rating: 5
Powered by Blogger.