AUNT LULU AJIBU HAYA KUFUATIA TUHUMA ZA KUWA NA VIRUSI VYA UKIMWI.

                                                                         Aunty Lulu.
Makubwa! Kufuatia fununu kuwa mwanadada asiyeishiwa matukio mjini, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ana ngoma na amejiunga kwenye kikundi cha watu waishio na virusi vya Ukimwi, mwenyewe amefunguka kwamba kama mtu ana uhakika ajitokeze waende pamoja wakapime.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita, Aunty Lulu alisema amekuwa akishutumiwa na watu kwamba ana ngoma jambo ambalo siyo kweli na mama yake ni shahidi kwani mapema mwaka huu walikwenda pamoja kupima na kukutwa yupo ‘biye’.
“Wanaonisema wanikome kabisa kwani hawana ushahidi na hawajawahi kunipima,” aling’aka Aunty Lulu.
AUNT LULU AJIBU HAYA KUFUATIA TUHUMA ZA KUWA NA VIRUSI VYA UKIMWI. AUNT LULU AJIBU HAYA KUFUATIA TUHUMA ZA KUWA NA VIRUSI VYA UKIMWI. Reviewed by Linnah Lsquare on 2:34 AM Rating: 5
Powered by Blogger.