NINI KIMEIKUMBA NDOA YA MAIMARTHA?SOMA MKASA MZIMA HAPA.

Mayasa Mariwata na Gladness Malya
Ooh…noo! Ile ndoa ya Mtangazaji Maimartha Jesse`Mai’ na mumewe, Raymond Shayo ‘Shaa’ inadaiwa kuwaka moto kufuatia ‘gogoro’ la ndani kwa ndani la mara kwa mara kwa wanandoa hao, kisa kikielezwa kwamba ni wivu uliokithiri wa mwanaume huyo.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na staa huyo, Shaa amefikia hatua ya kumkataza Mai kuhudhuria kwenye shughuli mbalimbali za mashosti zake na kujikuta akikaukiwa marafiki na kuishiwa ile shauku na utamu wa ndoa.
Alipotafutwa Mai na kusomewa ‘eituzedi’ ya sakata hilo alikuwa na haya ya kusema: “Nashindwa kulizungumzia si unajua mambo ya wanandoa ni siri? Ukweli mimi na mume wangu kuna kipindi huwa tunahitilafiana jambo ambalo ni kawaida katika ndoa,” alisema Mai.
NINI KIMEIKUMBA NDOA YA MAIMARTHA?SOMA MKASA MZIMA HAPA. NINI KIMEIKUMBA NDOA YA MAIMARTHA?SOMA MKASA MZIMA HAPA. Reviewed by Linnah Lsquare on 2:31 AM Rating: 5
Powered by Blogger.