AIBU! MKE AHARIBIWA SWAUMU NDANI YA DALADALA

Niaibu iliyoje! Licha ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, njemba mmoja ambaye jina lake halikufahamika, mkazi wa Raskazoni jijini hapa amepokea kichapo ‘hevi’ baada ya kumharibia swaumu mke wa mtu ndani ya daladala, Amani  lina kisa na mkasa.
Njemba huyo akipokea kichapo toka kwa abiria waliokuwemo kwenye daladala hiyo.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu na kuacha mshangao mkubwa kwa abiria huku wengine wakimwachia laana ya mdomo njemba huyo, lilijiri mapema wiki hii ndani ya dalalada inayofanya safari zake kati ya Sahare na Raskazoni ambapo mwanamke huyo alikosa siti hivyo akalazimika kusimama.
Shuhuda huyo alisema kuwa, ndani ya daladala hiyo kulikuwa na mbanano wa abiria ambapo njemba huyo alitumia fursa hiyo kujiridhisha baada ya kupata mfadhaiko kisha kumchafua mwanamke huyo aliyedai kuharibiwa swaumu yake kwa kuwa alikuwa amefunga.

...Wakizidi kumuadabisha.
“Jamaa tulimchukulia kama abiria wengine na kwa kuwa daladala ilikuwa imejaza sana, muda mwingi alionekana kumsogelea yule mke wa mtu na hatukujua kama alikuwa akitaka kumfanyia mchezo mbaya,aibu kweli” alisema shuhuda huyo.
Alitiririka kwamba, baada ya mwendo mrefu kidogo, njemba huyo alianza taratibu kufunua baibui la yule mke wa mtu na kuanza kumfanyia kitendo kichafu.
Mwanamke aliyefanyiwa kitendo hicho cha aibu akilia.
“Yule mke wa mtu mwanzoni aliona kawaida kugusana na abiria kutokana na gari kujaa lakini alikuja kushtuka kama anavuliwa nguo ndipo alipogeuka nyuma na kumkuta jamaa akiwa ameshikwa na mfadhaiko huku akiwa amemchafua nguo yake sehemu ya nyuma.
“Mke wa mtu ikabidi apige kelele ya kuhitaji msaada ndipo daladala ikasimama kituo cha Mabanda ya Papa na abiria wote tukamshusha na kuanza kumtembezea kichapo ambapo na yule mama alishindwa kujizuia na kuharibu swaumu yake kwa kumpiga,” alisema.
Hata hivyo, baada ya njemba huyo kupewa kichapo cha nguvu na raia waliomzingira, alifanikiwa kuchoropoka na kukimbilia eneo la ukuta na kutokomea akimuacha yule mama akiendelea kulia na kusema swaumu yake imeharibika.
AIBU! MKE AHARIBIWA SWAUMU NDANI YA DALADALA AIBU! MKE AHARIBIWA SWAUMU NDANI YA DALADALA Reviewed by Linnah Lsquare on 11:04 PM Rating: 5
Powered by Blogger.