WEMA NA MAIMARTHA WAFIKISHANA PABAYA.


Staa wa filamu, Wema Sepetu.
Mwandishi Wetu
KUMEKUCHA! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mtifuano kati ya mtangazaji maarufu wa televisheni, Maimartha Jesse na staa wa filamu, Wema Sepetu baada ya bifu la wawili hao kufika jeshi la polisi.

Mtangazaji maarufu wa televisheni, Maimartha Jesse.
Akipiga stori na gazeti hili, Maimartha alisema Wema alikuwa na nia ya kumdhalilisha kwani baada ya kumtafuta na polisi na kumkosa, waliamua kumpigia simu na kumuita kituoni Kijitonyama (Mabatini) ambako alisomewa mashtaka ya kumtukana Wema katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
“Yaani Wema alitaka kunidhalilisha ndiyo maana polisi walikuja kibao kwenye gari lao hapa dukani kwangu na waliponikosa ndiyo wakanipigia simu kwamba niende mwenyewe kituoni, nikaenda nikatoa maelezo yangu ila sasa nitakula naye sahani moja kwani watu wake wanaendelea kunitukana sana mtandaoni nami siwezi kukubali,” alisema Maimartha.
WEMA NA MAIMARTHA WAFIKISHANA PABAYA. WEMA NA MAIMARTHA WAFIKISHANA PABAYA. Reviewed by Linnah Lsquare on 11:45 PM Rating: 5
Powered by Blogger.