MAHARI YA WOLPER YAVUNJA REKODI.

Demu mkali wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ‘Jack’.
AMEPIGWA?! Mahari ya demu mkali wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ‘Jack’ inawezekana ikawa ndiyo ya kiwango cha juu kwa mastaa wa Bongo waliowahi kuolewa kwa utaratibu unaojulikana kihalali.
Chanzo chetu cha kuaminika kimesema na Amani kwamba, familia ya Wolper inataka mahari ya shilingi milioni 25 ikiwa ni ‘zawadi’ kwa wazazi wa staa huyo kukubali mtoto wao kuolewa na mchumba wake mwenye uraia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
“Mwanaume huyo alifurahishwa sana na wazazi wa Jack kumpokea vizuri. Nasikia kwenye eneo la mahari, wazazi wakataja kiasi hicho, kwamba kama jamaa atakuwa tayari ajiandae.
“Lakini pia, kuna vitu vingine ambavyo vinajumuishwa kwenye kuitwa mahari. Mfano, wanatakiwa ng’ombe wawili, mbuzi wawili, mashuka mawili au mablanketi na mapanga mawili,” kilisema chanzo. Katika kuonesha kuwa, ukiachia mbali mahari, harusi ya Wolper inaweza kuacha historia Bongo, inadaiwa itakuwa kwa siku saba ikianzia Dar (kwa kuwa ni makazi ya Wolper), Kibaha, Pwani (kwa wazazi) na Kilimanjaro (kwenye asili ya ukoo).
“Hiyo harusi itasherehekewa kwa siku saba ambapo itaanzia hapa Dar halafu Kibaha na itamaliziwa mkoani Kilimanjaro,” kilisema chanzo.Wakati hali ikitajwa kuwa hivyo, kuna habari kwamba, kati ya mambo ambayo Wolper anayakwepa kwa sasa ni kuwepo na habari ya mchepuko. Amekuwa akijichunga sana hata kujichanganya sehemu yenye starehe kama zamani anakwepa. Hataki kuharibu kabisa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye ndoa yake.
Gazeti hili lilimtafuta Wolper kwa ajili ya kufafanua madai hayo ili kubaini ukweli au kinyume chake ambapo alisema:
“Unajua mimi si msemaji wa familia. Kama ishu ni mahari kiasi hicho msemaji ni baba au mlipaji. Huko kujichunga na michepuko, mimi ni asili yangu. Inatokana na malezi yangu tangu utotoni.”
Hata hivyo, Wolper hakuwa tayari kutoa namba ya simu ya baba yake, mzee Wolper Masawe na wala hakuwa tayari kutaja namba za Mkongo wake huku baadhi ya watu wakisema kama ni kweli, jamaa atajifunza kitu kuhusu kuoa mastaa.
MAHARI YA WOLPER YAVUNJA REKODI. MAHARI YA WOLPER YAVUNJA REKODI. Reviewed by Linnah Lsquare on 12:02 AM Rating: 5
Powered by Blogger.