MASOGANGE NA DIVA NDANI YA BIFU ZITO KISA DAVIDO.

Na Imelda Mtema
KITUKO! Mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds, Loveness Malinzi ‘Diva’ na Video Queen maarufu Bongo Agness Jerald ‘Masongange’ wamejikuta wakiingia katika ugomvi, kisa kikiwa ni msanii wa muziki wa Nigeria, Davido.
Video Queen maarufu Bongo Agness Jerald ‘Masongange’.
Akizungumza na gazeti hili, Masogange alimlaumu Diva, kwa kitendo chake cha kuandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram kuwa alizungumza na Davido ambaye alikana kuwa na uhusiano na msichana yeyote kutoka Tanzania.
Mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds, Loveness Malinzi ‘Diva’.
“Kinachonishangaza kwanini Diva afikie hatua ya kumpigia mpaka Davido kumuuliza kuhusu uhusiano wangu na mwanamuziki huyo, kitu ambacho kimeshangaza hata msanii mwenyewe,”alisema Masogange.
Masogange alionesha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram meseji alizokuwa akimtumia mwanamuziki huyo, akishangazwa na dhamira ya swali hilo.“Inawezekana Diva anatafuta kiki kupitia jina langu, maana kila mtu anagombana naye, sasa huyo ni mtu wa aina gani jamani,” alisema Diva.
Diva, mmoja kati ya wanahabari wenye jina kubwa, alitafutwa kupitia simu yake ya kiganjani, lakini kwa muda mwingi iliita bila kupokelewa.
MASOGANGE NA DIVA NDANI YA BIFU ZITO KISA DAVIDO. MASOGANGE NA DIVA NDANI YA BIFU ZITO KISA DAVIDO. Reviewed by Linnah Lsquare on 2:58 AM Rating: 5
Powered by Blogger.