MASTAA WAMWANIKA MSHINDI WA URAIS

Mwandishi Wetu
UTAFITI uliofanywa na gazeti hili umeonesha mastaa wa muziki na filamu Bongo wanampa asilimia nyingi zaidi za ushindi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, John Magufuli dhidi ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.

Utafiti huo unaonesha, mastaa wengi wamejipambanua kuwa wanaiunga mkono CCM wakionesha kuguswa na sera za Magufuli huku wengine walikuwa wafuasi wa Chadema kinachoungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) lakini wamebadilika ghafla na kuingia CCM kutokana na kampeni ya Nimes’tuka.

Utafiti huo umebaini, wasanii wa filamu na muziki kama vile Stara Thomas, Jacob Steven (JB), Richie, Mike Sangu na wengine ambao wanazunguka mikoani na kampeni yao Kibajaj, wamewafikia watu wengi wakiwemo wasanii wenye majina makubwa na wasiofahamika sana ambao wamezielewa sera za Magufuli na kutangaza kumchagua.
Utafiti umebaini pia, kampeni ya Mama Ongea na Mwanao inayoongozwa na mwigizaji Wema Sepetu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Snura Mushi, Chuchu Hans, Wastara Juma, Salome Urassa ‘Thea’, Mayasa Mrisho ‘Maya’, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ na Maimartha Jesse wameongeza ushawishi mkubwa na watu kujiunga na CCM.

Utafiti huo umebainisha wasanii kama Aunt Ezekiel, Kajala Masanja, Vincent Kigosi ‘Ray’, Musa Kitale, Stan Bakora, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, Ali Kiba, Chegge, Aman Temba, Yamoto Band, Farid Kubanda ‘Fid Q’ na wengine kibao wapo upande wa CCM.
Kwa upande wa Chadema, utafiti umeonesha wasanii wachache kama Jacqueline Wolper, Raheem Nanji ‘Bob Junior’, Dayna Nyange, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Shamsa Ford, Ibrahim Musa ‘Roma’ na Kala Jeremiah.

Baada ya kuufikisha utafiti huo kwa timu ya Magufuli, imeelezwa kuwa umemshtua mgombea huyo na timu yake kwani umeonesha kumuacha mbali sana Lowassa huku pia ikielezwa umeishtua timu ya Lowassa ambayo ilikuwa ikiamini ina wasanii wengi zaidi wanaowaunga mkono.
MASTAA WAMWANIKA MSHINDI WA URAIS MASTAA WAMWANIKA MSHINDI WA URAIS Reviewed by Linnah Lsquare on 2:07 AM Rating: 5
Powered by Blogger.