SIJUI NDO LIMBWATA:DIAMOND HAFURUKUTI KWA ZARI

MWANDISHI WETU
Pamoja na kukanusha kwa nguvu zote, staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, anadaiwa kupandiwa kichwani na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ huku ndugu wakidaiwa kuhofia masuala ya kulishwa limbwata.
Staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Habari kutoka kwa mtu wa ndani wa familia ya Diamond zilidai kuwa, ishu hiyo imekuwa ‘hoti’ kiasi cha kuwatia hofu ndugu hao kwa sababu Zari akisema jambo lazima Diamond alitekeleze.“Hata ishu ya kuondoka kwenda kwao Afrika Kusini ‘Sauz’ akiwa na mtoto wao mchanga (Tiffah) ilikuwa ghafla sana na wala Diamond hakuweza kubisha.
“Kuna mambo mengine kibao ambayo Diamond alikuwa anamfanyia Zari ikiwemo kumpikia wakati yeye akichati kwenye simu na mambo mengine yanayofanana na hayo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
...Akipika.
“Asikwambie mtu, Diamond hafurukuti mbele ya Zari maana mwanamama huyo kampanda kichwani. Kuna wengine wanahusisha ‘situwesheni’ hiyo na umri maana Diamond katimiza umri wa miaka 26 juzikati wakati Zari kagonga 35.”
Akizungumzia hali hiyo, Diamond alifunguka kwa kifupi: “Nilishasema hayo ni mapenzi tu lakini Kibongobongo si unajua watu hawana dogo?”
SIJUI NDO LIMBWATA:DIAMOND HAFURUKUTI KWA ZARI SIJUI NDO LIMBWATA:DIAMOND HAFURUKUTI KWA ZARI Reviewed by Linnah Lsquare on 12:14 AM Rating: 5
Powered by Blogger.