ZITTO AMTWISHA MAGUFULI MAMBO 10 | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, November 11, 2015

ZITTO AMTWISHA MAGUFULI MAMBO 10

Mbunge Mteule wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.
Mbunge Mteule wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameelezea mambo 10 ambayo Rais Dk. John Magufuli, anapaswa kuyafanya ili kuweka misingi ya mabadiliko nchini.
Moja ya mambo ambayo ameandika kwenye waraka wake jana, Zitto amemshauri Rais Dk. Magufuli kuweka wazi mikataba yote  ya rasilimali za nchi.
"Kuna wakati Thomas Sankara (Rais wa zamani wa Burkinafaso) aliwahi kusema kwamba huwezi kuleta mabadiliko yoyote ya kweli kwa taifa kama hutakuwa na kiwango fulani cha wendawazimu,” alisema Zitto kwenye waraka huo.
Ushauri mwingine wa Zitto ni kwamba Dk. Magufuli afute posho zote za vikao katika mfumo mzima wa serikali kama mpango wa maendeleo unavyotaka
Amemshauri pia kufuta viongozi wa serikali na wanasiasa kusafiri kwa daraja la juu kwenye ndege isipokuwa Rais, Makamu wa Rais na  Waziri Mkuu. 
Zitto kwenye waraka huo pia amemshauri Dk. Magufuli kufuta matumizi ya mashangingi na aliisifu Benki Kuu ya Tanzania  (BoT) kwamba imeonyesha mfano kwenye hilo.
Pia alimshauri Rais Dk. Magufuli afute  uagizaji wa sukari kutoka nje na badala yake ianzishwe miradi ya miwa ili nchi iuze sukari Nje.
Jambo la sita aliloshauri Zitto ni kuweka weka wazi taarifa ya serikali kuhusu utoroshaji wa fedha na kufungua mashtaka dhidi ya wahusika mara moja.
Alisema Dk. Magufuli anapaswa kuipa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa  (Takukuru)  mamlaka ya kukamata na kushtaki na kila mwenye mali athibitishe mwenyewe ameipataje.
Alisema mali na madeni ya viongozi yawe wazi kwa umma na wananchi waruhusiwe kuhoji.
Katika jambo la tisa, Zitto alimshauri Dk. Magufuli  kuruhusu mshindi wa uchaguzi Zanzibar atangazwe na afanye naye kazi.
Zitto katika ushauri wake wa mwisho alimtaka  Rais Dk. Magufuli kuendelea na  mchakato wa Katiba kwa kuanzia alipoishia Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na kuachana na Katiba Pendekezwa.
CHANZO: NIPASHE

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers