Hii Ndio Sababu Kwanini Mwanamuziki Jux Hapendi Kumuongelea Mpenzi Wake wa Zamani Jack Cliff Aliyoko Jela China | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Wednesday, February 17, 2016

Hii Ndio Sababu Kwanini Mwanamuziki Jux Hapendi Kumuongelea Mpenzi Wake wa Zamani Jack Cliff Aliyoko Jela China

Msanii mahiri wa miondoko ya R&B amekuwa hapendi kuzungumzia suala la mpenzi wake wa zamani Jack Patrick ambaye anatumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong nchini China kwa tuhuma za kugundulika na madawa ya kulevya katika mwili wake.

Jux amekuwa akiulizwa mara kadhaa na waandishi wa habari kuhusu suala hilo lakini amekuwa hataki kulizungumzia suala hilo lakini kupitia kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds Fm Radio amefungukia suala hilo na kusema kuwa hapendi kulizungumzia suala hilo ili asije akaonekana anapatia umaarufu au kiki kupitia yaliyo msibu mpenzi wake.


Jux ameongeza kuwa siyo vizuri kulizungumzia suala hilo kwani atandugu zake Jack hawapendi, hivyo anapenda kuulizwa zaidi kuhusu kazi zake anazo zifanya, huku akisisitiza kuwa kwa sasa ana mpenzi ambaye anampenda kwa dhati na ikitokea x-wake akaachiwa itabidi akubaliane na atakayo yakuta.

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers