FAIDA ZA MAJI YA MATUNDA | Bongo Voice
Breaking News
Loading...

Tuesday, May 24, 2016

FAIDA ZA MAJI YA MATUNDA


Leo kwenye urembo nitaongelea suala zima la kuwa na ngozi nzuri yenye mvuto ambayo utaipata kwa kunywa maji ya matunda.
Kama tulivyozoea, maji ya kunywa huwa yanatajwa kwenye kuing’arisha ngozi na kuondoa sumu mwilini. Sasa leo nitakufundisha jinsi ya kunywa maji mengi zaidi ambapo utatumia na matunda ili kuipata ngozi nyororo.
Chukua jagi lako la maji safi ya kunywa, changanya na limao na ndimu, vyote na maganda yake, weka pamoja na vipande viwili vya tango.
Hapa nikiongelea matunda simaanishi juisi yake bali namaanisha vipande ambavyo havijakatwa vya matunda hayo.
Hatua ya kwanza ni kuchanganya na maji hayo, hatua ya pili ni kuweka kwenye friji au pembeni yake kwa muda wa masaa 8 kupata ile ladha kisha ndiyo uanze kunywa.
Faida ya maji haya ya matunda
Kwanza; yanakusaidia kunywa maji kwa urahisi kwani yatakuwa na harufu nzuri na ladha inayonyweka zaidi ya maji matupu.
Pili; inasaidia kupunguza tumbo kwa wale wasiopenda matumbo makubwa.
Tatu;  Yanasaidia kukupa ngozi nyororo yenye kutelezea.
Kama utakosa matunda hayo, unaweza kutumia zabibu, tikiti maji, chungwa na strawberry

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT

 

Google+ Badge

Google+ Followers