Bakwata Lawakana Mashehe Walioenda Kanisani kwa Gwajima

Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) limetoa tamko kuhusu picha za mashehe zinazoendelea kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii, zikiwaonesha wakiwa kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo Dar linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, na kueleza kuwa mashehe hao hawana uhusiano wowote wa Bakwata na hata ziara yao kanisani hapo, haikuwa na baraka zao.

 Katika taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Bakwata, Horera Tabu, imeeleza mashehe hao hawana uhusiano wowote na Bakwata na kuongeza kuwa Watanzania wanashauriwa kuendelea kuliombea taifa letu liweze kudumu katika hali ya utulivu na amani.
Katika ibada ya Jumapili iliyopita kanisani kwa Gwajima, wanaume kadhaa waliovalia kanzu na baraghashia, ambao walitambulishwa kama mashehe, walihudhuria kanisani hapo kama wageni waalikwa, sambamba na wachekeshaji Mkude Simba na Stan Bakora
Bakwata Lawakana Mashehe Walioenda Kanisani kwa Gwajima Bakwata Lawakana Mashehe Walioenda Kanisani kwa Gwajima Reviewed by Linnah Lsquare on 5:39 AM Rating: 5
Powered by Blogger.