Maswali Zaidi ya 1000 Yakosa Majibu Kuhusu Kutekwa na Kuachiwa kwa Roma Mkatoliki ..!!

Yanaweza yakafika maswali 1,000. Mijini na vijijini watu wanajiuliza maswali na kama kila swali litachukuliwa kwa uzito, Roma Mkatoliki atakuwa na kazi ya kujibu zaidi ya maswali 1,000 ya Watanzania.
Baadhi ya maswali  ambayo hayajapata majibu kuhusu utekaji wa Roma ni pamoja na alichohojiwa na watekaji, kwa nini watekaji waliwafunga vitambaa vyeusi, kwa nini ofisa mmoja wa Serikali alitabiri kuwa watarudi kabla ya Jumapili na utata kuhusu mazingira ya kufika polisi baada ya kutekwa.
Siku moja baada ya kuachiwa na watekaji, Roma hakueleza alichohojiwa na watekaji. “Watekaji walikuwa wakituhoji na kutupiga,” alisema Roma aliyekuwa amefuatana na wasanii aliotekwa nao, Moni, Bin Laden na Imma.
Mchambuzi wa masuala ya siasa na jamii, Godlisten Malisa ameandika katika mtandao wake wa facebook akihoji maswali kadhaa kuhusu utekaji wa Roma.
Miongoni mwake anahoji, ni kwa nini msanii huyo alijikuta yupo Ununio, lakini akaenda kuripoti Kituo cha Polisi Kati (kikuu) na baadaye Oysterbay huku akiwa tayari amekwenda nyumbani kwake kubadilisha nguo ambazo ni ushahidi badala ya kwenda polisi moja kwa moja.
Swali hilo ambalo majibu yake hayajapatikana linapewa nguvu na idadi ya vituo vya polisi vilivyopo kati ya Ununio na Posta, ambayo Roma alivipita bila kujisalimisha na kutoa taarifa kuwa alikuwa ametekwa.
Maswali Zaidi ya 1000 Yakosa Majibu Kuhusu Kutekwa na Kuachiwa kwa Roma Mkatoliki ..!! Maswali Zaidi ya 1000 Yakosa Majibu Kuhusu Kutekwa na Kuachiwa kwa Roma Mkatoliki ..!! Reviewed by Linnah Lsquare on 6:44 AM Rating: 5
Powered by Blogger.