Wabunge 'Wasasambuana' Bungeni..Ni Kuhusu Ripoti Hii ya Twaweza..!!!

Hatimaye mvutano wa wabunge wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) na Chadema umehamia katika ripoti ya utafiti kuhusu masuala ya kielimu uliokuwa ukitolewa na shirika lisilo la kiserikali la Twaweza.
Wabunge wa Chadema walichangia kwa kueleza namna Serikali ilivyoshindwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na walimu hasa wa sayansi.
Mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Chacha amesema Serikali imeitelekeza elimu na kuwafanya vijana wa Kitanzania waishi kwa kupata elimu ya kubahatisha.
Hata hivyo, wabunge wa CCM, Hawa Ghasia na Fatuma Tawfiq ambao walijibu kuwa kauli za wabunge wa Chadema  ni za uchochezi kwa kuwa Serikali imekuwa ikifanya mambo yake kwa utaratibu na ubora wa hali ya juu.
Awali, Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Eyakuze aliwaambia wabunge kuwa hali bado ni mbaya kwa wanafunzi wa Kitanzania hasa shule za msingi.
Wabunge 'Wasasambuana' Bungeni..Ni Kuhusu Ripoti Hii ya Twaweza..!!! Wabunge 'Wasasambuana' Bungeni..Ni Kuhusu Ripoti Hii ya Twaweza..!!! Reviewed by Linnah Lsquare on 12:18 AM Rating: 5
Powered by Blogger.