MSIBA: MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA!

Sudi Mohamed, 'MCD' (pichani, juu na chini) ambaye ni mpinga tumba maarufu nchini Tanzania amefariki dunia usiku huu akiwa Moshi ambako alikwenda kwa ajili ya matiabu zaidi yapata miezi mitatu iliyopita. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Meneja Hassani, MCD alipelekewa nauli ya kurudi jijini Dar esalaam leo ili arejee kesho lakini mauti yakamfika usiku mida ya saa tano na nusu. MCD amewahi kupiga katika bendi kadhaa za muziki wa dansi ikiwemo Mashujaa Band na African Stars ambako alirejea tena. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - ameen!

MSIBA: MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA! MSIBA: MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA! Reviewed by Linnah Lsquare on 9:42 PM Rating: 5
Powered by Blogger.